Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi amewakabidhi Vyeti na Fedha Taslim Jumla ya Wafanyakazi Saba (7) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika Kitaifa Dole Mkoa wa Mjini Unguja.
Wafanyakazi waliokabidhiwa zawadi hizo ni pamoja na Mha. Joseph R. Mabagala (Mkaguzi Mafuta), Ali S. Ali (Afisa TEHAMA Msaidizi), Aisha J. Hassanali (Katibu Muhtasi), Mha. Abubakar B. Omar (Mkaguzi Mafuta Pemba) Mwanaidi S. Abdullah (Muhudumu) Othman A. Suleiman (Karani) na Rahma H. Thabit ( Afisa Uhusiano)
ZURA ni miongoni mwa Taasisi ya Umma inayojenga weledi kwa Wafanyakazi wake ambapo kila Mwaka hutoa Wafanyakazi bora.




