Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) inashiriki katika Maonesho ya Wafanyakazi Duniani yanayofanyika Dimani Dole Zanzibar kuanzia Tarehe 27/04/2026 mpaka 05/05/2026.
Maonesho hayo yameandaliwa na Chama cha Wafanyakazi (ZATUC) yalifunguliwa na Waziri wa Biashara na Viwanda Ndg. Sharif Ali Sharif na kufungwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Maonesho hayo yamelenga kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo yana Kauli mbiu “Upatikanaji wa haki, maslahi na mazingira bora kazini ni msingi wa uwajibikaji, nidham na maadili ya wafanyakazi”
Aidha, ZURA kupitia Maonesho kama hayo inapata nafasi ya kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Mafuta na Gesi na kutoa elimu kwa Wananchi juu ya huduma inazozidhibiti zikiwemo Maji, Umeme, Mafuta pamoja na Gesi ya kupikia (LPG).
Kupitia Maonesho haya, Mamlaka inapata fursa ya kukutana na Wananchi na Wafanyakazi kwa kutoa elimu kwa wadau wake wanaotembelea katika banda lake kujifunza kuhusu masuala ya udhibiti wa sekta ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi.
Mamlaka inashiriki katika Maonesho ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yanayofanyika Dimani dole Zanzibar kuanzia Tarehe 27/04/2026 mpaka Tarehe 05/05/2026
Miongoni mwa Washiriki wa Maoneosho haya ni pamoja na ZURA, ZAA, ZRA, ZBS, ZPDC, ZPC,BPRA, PBZ, ZCT, ZASCO, BOT, ZSSF, na Wajasiriamali.



