Mamlaka ya Udhubiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) inashiriki katika Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika Dole-Kizimbani Zanzibar kuanzia Tarehe 01/08/2025 mpaka Tarehe 14/08/2024.
ZURA inayatumia Maonesho hayo kama fursa ya kukutana na Wananchi na kutoa elimu kwa wadau wake wanaotembelea katika banda lake kujifunza kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi.
ZURA pia inapata fursa ya kuongeza idadi ya Wawekezaji katika sekta za Maji na Nishati kwa vile wawekezaji wengi hutembelea na kuelezwa fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar.
Miongoni mwa Washirki wa Maonesho haya ni pamoja na ZURA, TANTRED, CRDB, PBZ, PSSF, ZSSF, BPRA, ZASCO, ZBS, ZRA, BOT,ZRA, ZCT na Wajasiriamali
ZURA hushiriki katika Maonesh ili kupata kukutana na Wananchi na kutoa elimu kuhusu masuala ya udhibiti wa sekta ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi pamoja na kupokea maoni na changamoto za huduma hizo na kuzipatia ufumbuzi.

