Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imeshiriki katika ufunguzi wa kituo cha kujazia gesi ya kupikia kwenye Magari (LPG Auto Gas Station) uliofanyika katika Bohari ya Kampuni ya ORYX Mangapwani Mkoa wa Kasakazini Unguja.
Kituo hicho ni cha kwanza kufunguliwa Zanzibar na kina lengo la kuwasaidia wananchi wanaotumia Gari zinazoendeshwa kwa kutumia gesi kupata huduma hiyo, kwavile hakukuwa na Kituo kama hicho awali.
Lengo jengjne la kufunguliwa Kituo hicho ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamisha matumizi ya Nishati rafiki wa Mazingira, kupunguza uzalishaji wa mosho unaopelekea uharibifu wa mazingira kwa kupelekea mabadiliko ya Tabia Nchi.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZURA ambayo ipo chini ya Wizara ya Maji, Nishati na Madini imekua ikihamasisha matumizi ya gesi ya kupikia (L.P.G) ikiwa ni pamoja na kutumika kwenye magari.
ZURA hudhibiti Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ikiwemo Gesi kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zina ubora unaokubalika, zinapatikana kwa kiwango kinachohitajika na gharama inayostahiki.

