ZURA YAPONGEZWA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

  • Home
  • ZURA
  • ZURA YAPONGEZWA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imepongezwa na Viongozi waliotembelea Banda la ZURA kwa kutoa elimu na kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya maji na nishati.

Pongezi hizo zilitolewa katika Jengo la Zanzibar katika Maonesho ya Maonesho ya 49 ya Biashara Dar es salaam (Sabasaba) ambapo Banda la ZURA linapatikana ndani yeke.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstafu ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa Viongozi walioipongeza ZURA kwa kutoa elimu kwa jmii hasa kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi.

ZURA inayatumia Maonesho haya kama fursa ya kuongeza idadi ya wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati kwavile wawekezaji wengi hutembelea na kuelezwa fursa za uwekezaji zilizopo Zanizibar.

Kupitia Maonesho haya, ZURA pia ilipata fursa ya kukutana na Wananchi na kutoa elimu kwa wadau wake wanaotembelea katika banda lake kujifunza kuhusu masuala ya udhibiti wa sekta ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi.

ZURA ilishiriki katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam (Sabasaba) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalim Julius Nyerere (Viwanja vya Sabasaba) Temeke, Dar es salam kuanzia Tarehe 28/06/2024 mpaka Tarehe 13/07/2024.

Maonesho hayo yalifungwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaaliwa Majaaliwa, ambapo miongoni mwa Washiriki wa Maoneosho haya kutoka Zanzibar ni pamoja na ZURA, ZAA, ZRA, ZBS, ZPDC, ZPC,BPRA, PBZ, ZCT, ZASCO, ZSSF, na Wajasiriamali.

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.