ZURA YAKUTANA NA WATUMIAJI WA ENEO LA BOHARI YA MAFUTA – MTONI

  • Home
  • ZURA
  • ZURA YAKUTANA NA WATUMIAJI WA ENEO LA BOHARI YA MAFUTA – MTONI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya kikao na wadau wanaotumia eneo Bohari ya Mafuta Mtoni, Unguja.

Kikao hicho kimefanyika katika eneo la Bahari ya Mtoni Unguja pembezoni mwa Bohari ya Mafuta na kuwakutanisha wadau wakiwemo Wavuvi, Shirika la Bandari, Wizara ya Uchumi wa Buluu, Wilaya ya Mjini na Shirika la Meli.

Lengo la mkutano huo ni ili kuweka mipaka ya matumizi na kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo la Bohari ya Mafuta Mtoni, ikiwa ni pamoja na kutoruhusu shughuli za kijamii kufanyika katika eneo hilo kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza.

Mkurugenzi Mkuu ZURA, Nd. Omar Ali Yussuf akifungua kikao hicho aliwataka wadau kutoa mapendekezo yao kwa kuzingatia usalama wa wananchi na mali zao.

Aidha, Mkurugenzi Omar aliwataka wadau wengine wa Serekali kutoa mapendekezo yao ili kufanikisha zoezi la uwekaji wa mipaka katika eneo la bahari ya Mtoni.

Nae kwa upande wake, Mkurugenzi Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) Nd. Akif Ali Khamis aliwaelekeza wavuvi kuwa mapendekezo yao yatafanyiwa kazi kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo hilo.

Aidha, Wadau waliiomba kutengewa eneo maalum la Bandari ya Majahazi ili kurahisisha kazi zao za kila siku, ambapo Uongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) ulipokea na kuahidi kuyafanyia kazi.

ZURA ina kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara kwa ajili ya kujadili masuala yanohusiana na huduma ya Maji na Nishati na kuwapa fursa ya kutoa maoni , kuuliza maswali na kuwasilisha changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi.

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.