Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya kikao na wadau wa Mafuta kwa lengo la kujadili Mpango wa Utekeleza wa Mfumo wa Uingizaji Mafuta kwa Jumla (BPS Impelentation Manual) kwa mwaka 2025, Makao Makuu ya ZURA Maisara, Unguja.
Akiwasilisha utekelezaji huo Kaimu Meneja Kitengo cha Usimamazi wa Uletaji wa Mafuta kwa pamoja ZURA Mha. Jabir Shaib Is’haka amewataka wadau waliopata fursa ya kushiriki kikao hicho kutoa maoni na ushauri juu mpango huo ili kuleta ufanisi wa kazi zao.
Miongoni mwa washiriki wa kikao cha Utekelezaji wa mfumo wa Uingizaji wa mafuta ni Kampuni ya UP, GAPCO, ZP, PUMA na GBP pamoja na Taasisi za Serikali ikiwemo TRA, ZRA, ZAWEMA na KZU ambao walipata fursa ya kutoa michango kuhusiana na mpango huo.
Mpango wa Utekeleza wa Mfumo wa Uingizaji Mafuta kwa Jumla (BPS Impelentation Manual) kwa mwaka 2025 unatajiwa kuwa muongozo thabiti wa uletaji na ushushaji wa Mafuta Unguja na Pemba, na iwapo utafutwa kikamilifu utahakikisha upatikanaji wa bidhaa za Mafuta muda wote.
Mamlaka ina kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara kwa ajili ya kujadili masuala yanohusiana na huduma ya Maji na Nishati na kuwapa fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kuwasilisha changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wao wa kazi.

