Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi amewakabidhi Vyeti na fedha Taslim Jumla ya Wafanyakazi watano (5) wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika Kitaifa Nyamanzi Mkoa wa Kusini Unguja.
Wafanyakazi waliokqbidhiwa zawadi hizo ni pamoja na Ali Abdalla Ali Mkaguzi mafuta, Ali Salum Moh’d Dereva, Samia Yussuf Moh’d Karani, Rajab Said Moh’d Mkaguzi Maji.
ZURA ni miongoni mwa Taasisi za Umma inayojenga weledi wa Wafanyakazi wake ambapo kila Mwaka hutoa Wafanyakazi bora.

