ZURA YAFANYA UKAGUZI WA UMEME MKOA WA KUSINI

Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa ubora wa huduma ya Umeme kwa kukagua Transfoma za usambazaji wa Umeme majumbani katika Mkoa wa kusini Unguja. Mamlaka imefanya ukaguzi huo tarehe 13 Septemba 2023 kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika maeneo…

ZURA YAKUTANA NA PBZ

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya kikao kifupi na Bank ya Watu wa Zanzibar (PBZ) lengo ni kuimarisha ushirikiano baina yao. Aidha kikao hicho kilifanyika maisara ZURA Leo tarehe 08/08/2023.

ZURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA ZANZIBAR.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza Bei mpya za Mafuta kwa Mwezi wa Septemba 2023 ambazo zitaanza kutumika rasmi Siku ya Jumamosi Tarehe 09/09/2023. Bei zilizotangazwa kwa Mwezi Septemba ni kama zifuatazo Petroli TZS 2,950, Dizeli TZS 3,012, Mafuta ya Taa TZS 2,921 na…

ZURA NA EWURA YAFANYA KIKAO KAZI KUPANGA BEI ZA MAJI NA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya Kikao kazi na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ili kubadilishana uzoefu wa upangaji wa bei za Maji na Umeme kufuatia mabadiliko ya mifumo ya utendaji kazi wa Mamlaka hizo. Mkurugenzi Mkuu – ZURA…

ZURA YATOA MSAADA WA VITENDEKEA KAZI KWA WASAIDIZI WA SHERIA ZANZIBAR.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetoa msaada wa vitendea kazi kwa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora. Vitendea kazi hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu (ZURA) Ndg. Omar Ali Yussuf kwa lengo kusambazwa kwa Wasaidizi wa Sheria Zanzibar katika Wilaya zote Unguja na…

BEI MPYA ZA MAFUTA ZATANGAZWA 

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ndg. Mbarak Hassan Haji ametangaza Bei Mpya za Mafuta Leo Tarehe 08/08/2023 katika Ukumbi wa ZURA, Maisara Unguja. Bei hizo zilizotangazwa Leo zitaanza kutumika rasmi kuanzia Kesho Siku ya Jumatano Tarehe 09/08/2023 ni: PETROLI: TZS 2,970/LITA…

MKURUGENZI MKUU – ZURA ATEMBELEA MAONESHO 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Ndg. Omar Ali Yussuf ametembelea Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) yanayoendelea Dole – Kizimbani, Zanzibar tangu Tarehe 01/08/2023 mpaka Tarehe 10/08/2023. Mkurugenzi Omar ametembelea mabanda tofauti yakiwemo banda la  Wakulima, Kampuni ya Oryx na Kamisheni ya…