Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya ukaguzi wa Kituo kipya kinachoendelea na ujenzi cha Kigomasha kilichopo Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ukaguzi wa Kituo hicho ni hatua za kuifanyiakazi kanuni ya usimamizi wa Vituo vya Mafuta ya 2022 ili kuwa na Udhibiti bora wa Vituo vya Mafuta Nchini.
Akizugumza katika Ukaguzi wa kituo hicho kilicho katika hatua ya Mwisho (Finishing) Mkaguzi Mafuta na Gesi ZURA Nd. Said Ali Makame amesema ujenzi wa kituo hicho unaendelea kufuata kanuni za Mamlaka utatanua wigo wa upatikanaji huduma ya Mafuta kwa Wananchi wa Makangale na Vitongoji vyake.
Mhandisi wa Kituo hicho Mha. Suleiman Khamis Saleh amesema ujenzi wa Kituo hicho umezingatia ubora na usalama wa Mazingira na Watumiaji wa Kituo icho ili kuweza kutua huduma ya uhakika.
Mamlaka inakawaida ya Kivikagua Vituo vipya vya Mafuta Vinavojengwa Unguja na Pemba kuanzia hatua ya awali hadi kukamilika kwake kwa lengo la kuhakikisha Vituo hivo vinafuata kanuni na miongozo ya Mamlaka.

