ZURA YAANDAA KANUNI YA UBORA WA UMEME

  • Home
  • ZECO
  • ZURA YAANDAA KANUNI YA UBORA WA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) kupitia Mradi wa ZESTA imefanya kikao na Wadau wa Umeme kwa lengo la kujadili Kanuni ya Ubora wa Huduma ya Umeme Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Madinat Al Bahr kikijumuisha Wadau kutoka Taasisi za Serikali zikiwemo ZECO, ZAWEMA, ZBS na WMNM pamoja na wadau binafsi wakiwepo Hoteli ya Baraza Resort Zanzibar.

Aidha, kikao hicho kiliwataka wadau kutoa mapendekezo, maoni pamoja na kuiangalia Kanuni hiyo ili kujenga njia nzuri za utoaji wa huduma kwa wateja wanaotumia huduma.

Akiwasilisha Rasimu ya kanuni hiyo Mkaguzi Umeme ZURA Mha. Khamis Ali Khamis aliwataka watoa huduma hao kusimamia huduma zinazotolewa na kuhakikisha wanafuata yale yote yaliomo katika kanuni hiyo.

Mamlaka ina kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara kwa ajili ya kujadili masuala yanohusiana na huduma ya Maji na Nishati na kuwapa fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kuwasilisha changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wao wa kazi na Mamlaka kuahidi kuzifanyia kazi.

Archives

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)