Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imkutana na JICA kwa lengo la kujadili Maendeleo ya Mradi wa Usimamizi wa Vyanzo vya Maji kikao kilichofanyika Leo Tarehe 19/05/2025 Makao Makuu ya ZURA Maisara. Unguja.
Akifungua kikao Mrugenzi Mkuu ZURA Nd. Omar Ali Yussuf amesema Mamlaka ipo tayari kuendeleza mashirikiano na JICA ili kuleta ufanisi mzuri wa kazi na Sekta ambazo zinadhibitiwa na ZURA ikiwemo Maji na Nishati.
Kawaida ZURA hufanya vikao na Wadau kwa lengo la kuendeleza ushirikiano na kuwa endelevu kwa taasisi ya ZURA katika kuimarisha utekelezaji wa Miradi kwa watoa huduma za Maji na Nishati.

