ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA 2024

ZURA YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) inashiriki katika Maonesho ya Biashara kuadhimisha miaka 60 Muungano wa Tanzania.

Maonesho hayo yanafanyika Nyamanzi Unguja kuanzia tarehe 14/04/2024 mpaka tarehe 20/04/2024 na kushirikisha Wajasiriamali wa kisiwa cha Unguja pamoja na Taasisi za Serikali.

Maonesho hayo yamefunguliwa na Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi  pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali.

Mamlaka inashiriki katika Maonesho ya Muungano ili kuunga mkono juhudi za serikali na Wajasiriamali ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka, pia  kuuenzi na kuendeleza Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mamlaka inatoa elimu kwa wananchi wanaotembelea Maonesho hayo na kuskiliza changamoto za wananchi. Pia inatangaza fursa kwa Wawekezaji katika Sekta za Maji na Nishati wanaotembelea Maonesho hayo.

Maonesho ya Muungano yameandaliwa na  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kwa lengo la kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.