ZURA YASHIRIKI ZIARA YA NAIBU WAZIRI WMNM PEMBA

ZURA YASHIRIKI ZIARA YA NAIBU WAZIRI WMNM PEMBA

Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) wameshiriki ziara ya kusikiliza changamoto na malalamiko juu ya upatikanaji wa huduma ya Maji na Umeme kisiwani Pemba.
Mamlaka imeshiriki ziara hiyo kuanzia Alhamis ya Tarehe 28/03/2024 hadi Jumatatu Tarehe 01/04/2024 iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Zawadi Amour Nassor kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Mamlaka imeshiriki Ziara hiyo katika Wilaya ya Micheweni, Wete, Chakechake na Mkoani kwa lengo la kusikiliza na kutatuwa changamoto hizo pamoja na kugawa Maji safi kwa Wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
ZURA imeitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kufanyia kazi baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika Vijiji vya Kisiwa cha Pemba vilivyofanyiwa Ziara ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya wa maji safi na salama katika Vijiji hivyo.
ZURA hushiriki Ziara  kila inapohitajika kwa lengo la kuimarisha huduma ya Maji, Umeme, Mafuta na Gesi kwa Wananchi wake ili kuhakikisha huduma hizo zinapatikana kwa ubora na uhakika Unguja na Pemba.