ZURA YAKUTANA NA WADAU WA MAFUTA PEMBA

  • Home
  • ZURA
  • ZURA YAKUTANA NA WADAU WA MAFUTA PEMBA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya kikao na wadau wa  Vituo vya Mafuta Pemba kwa lengo la kusikiliza changamoto zao.

Kikao hicho kimefanyika Tibirinzi katika Ofisi za ZURA Tawi la Pemba kwa kauwakutanisha wadau wote wa Vituo vya Mafuta wakiwemo Wamiliki wa Vituo hivyo.

Mkurugenzi Mkuu ZURA, Nd. Omar Ali Yussuf akifungua kikao hicho aliwataka wadau kueleza changamoto zao kwa lengo la kuimarisha huduma bora za mafuta kisiwani Pemba.

Mkurugenzi Omar aliwaahidi wadau hao kuwa Mamlaka itahakikisha inatatua changamoto zao kwa wakati ili kuhakikisha huduma ya mafuta inapatika muda wote bila ya usumbufu.

Aidha, Mkurugenzi Omar aliwataka watendaji wa Mamlaka kuhakikisha wanafuata Sheria, Kanuni na Miongozo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Miongoni mwa washiriki wa kikao hicho ni Kampuni ya GAPCO (Bohari ya Pemba), Meneja wa Vituo vya Mafuta Pemba ambao walipata fursa ya kutoa michango na kueleza changamoto zao.

ZURA ina kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara kwa ajili ya kujadili masuala yanohusiana na huduma ya Maji na Nishati na kuwapa fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kuwasilisha changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi.

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.